KUZIONA TANZANITE, NIGERIA 500 TU
Na Saida Salum. Dar es Salaam
TFF imetoa fursa ya mashabiki wengi kuingia uwanjani kuishangilia Timu ya Taifa ya Wanawake wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ itakayocheza kesho na Falconets ya Nigeria kwa kuweka kiingilio cha shilingi 500 pekee.
Katika mchezo huo utakaofanyika dimba la Azam Complex Chamazi, kiingilio cha shilingi 500 kitakuwa kwa mashabiki watakaoketi eneo la mzunguko huku kwa wale watakaokaa Jukwaa Kuu (VIP) watalipia Shilingi 1,000 pekee