YANGA BUTU YALAZIMISHWA SARE NA MTIBWA SUGAR
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Hali si nzuri kwa mabingwa wa soka nchini baada ya kulazimishwa sare tasa na vinara wa ligi hiyo Mtibwa Sugar jioni ya leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Yanga inaonekana wazi kufeli kwenye idara yake ya ushambuliaji kwani imekosa mabao manne ya wazi ambayo yamemfanya kipa wa Mtibwa Sugar, Bennedictor Tinoco kuonekana bora, lawama nyingi zimemuendea Mzimbabwe Donald Ngoma kwa kutokuwa makini na kuifanya Yanga itoke kapa.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 9 ikiwa imecheza mechi tano ikifanikiwa kushinda mechi mbili, sare tatu, wakati Mtibwa Sugar wanaendelea kushikilia usukani wa ligi hiyo wakifikisha pointi 11 baada ya mechi tano, nne tatu wakishinda na mbili kwenda sare