Ukweli kuhusu Chirwa kumpiga mwandishi huu hapa
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Ukweli umebainika baada ya mshambuliaji wa Yanga Mzambia, Obrey Chirwa kutaka kumshambulia mwandishi wa gazeti la Mtanzania, John Dande umewekwa hadharani na mmoja wa waandishi ambaye hakutaka kutaja jina lake.
Taarifa zimebainika kuwa mwandishi huyo akiwa na kamera yake alimfuata Chirwa ambaye alikuwa anabadilisha nguo ili aanze mazoezi, mwandishi huyo inadaiwa alimpiga picha hiyo ambayo Chirwa hakuridhika na kumfuata kisha kumpa kisago kabla ya Juma Abdul naye wa Yanga kuingilia kati.
Hata hivyo mwandishi huyo alizifuta picha hizo baada ya Chirwa kumtaka afanye hivyo, Vyombo vya habari vimepinga vikali kitendo hicho cha Chirwa kumpiga mwandishi huyo.
Lakini Mambo Uwanjani ilizungumza na mwandishi huyo ambapo alisema yamekwisha na ameshamsamehe mchezaji huyo ingawa alidai alimpiga picha ya uwabjani na si akibadilisha nguo kama inavyoelezwa