Kocha wa Njombe Mji abwaga manyanga
Na Exipeditor Mataruma. Songea
Kocha mkuu wa Njombe Mji FC ya Njombe, Hassan Banyai ameamua kubwaga manyanga baada ya mwenendo mbaya wa timu yake kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Banyai amejiuzuru baada ya timu yake kupoteza mechi zote tatu ilizocheza hadi sasa, kocha huyo aliyewahi kuzinoa Moro United na Majimaji ameamua kuacha kazi ili kumpisha kocha mwingine aweze kuwasaidia.
Njombe Mji FC imefungwa mechi zote tatu za Ligi Kuu Bara, kitendo hicho kimepelekea kocha huyo kujiuzuru ili kulinda heshima yake kwani bado timu hiyo itaendelea kushindana na inaweza ku