SIMBA MGUU SAWA KWA MBAO KESHO

Na Paskal Beatus. Mwanza

Kikosi cha Simba kipo tayari kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji wao Mbao FC utakaopigwa kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Simba iliwasiri Mwanza jana ikitokea Dar es Salaam ambapo iliifunga Mwadui FC ya Shinyanga mabao 3-0 huku Mbao FC ikitoka kupokea kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mjini Morogoro hivyo mchezo wa kesho utakuwa mkali kwani Mbao hawatakubali kuendelea kupoteza mechi zake.

Mbao FC wana kumbukumbu ya kufungwa na Simba mara mbili tatu ilizokutana, mara mbili kwenye Ligi Kuu na mara moja kwenye mchezo wa fainali ya kombe la FA, hivyo mchezo wa kesho utakuwa mgumu kwa timu mbili, Simba nao wanataka kushinda ili kukaa kileleni

Simba wakiomba dua, kesho wanakutana na Mbao FC

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA