Simba yalazimishwa sare na kitimu kisichojulikana
Na Mwandishi Wetu. Tabora
Simba SC jioni ya leo imeshindwa kutamba mbele ya kitimu cha daraja la pili, Milambo FC baada ya kutoka suluhu 0-0 mchezo wa kirafiki katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mabingwa hao wa Ngao ya Hisani walishindwa kabisa kutawala eneo la kiungo licha ya kushusha kikosi chake chote ambacho kikajikuta kinakamatwa na wasiojulikana hao wa Milambo ambao wanatafuta nafasi ya kurejea Ligi Kuu Bara tangu enzi za Rais Benjamin Mkapa walipokuwa wanashiriki ligi hiyo, Simba wapo Tabora kwa maandalizi ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Stand United.
Simba leo ilimchezesha kwa mara ya kwanza kiungo wake Jonas Mkude ambaye alianza mwanzo hadi mwisho akisaidiana na Mnyarwanda Haruna Niyonzima ambaye alishindwa kufurukuta mbele ya vijana hao wasiojulikana wa Milambo