Singida United yaipigia hesabu kali Azam FC
Na Paskal Beatus. Dodoma
Kocha mkuu wa Singida United, Hans Van der Pluijm raia wa Uholanzi amesema kwa sasa hesabu zao wanazielekeza kwa Azam FC ambao watapambana nao mwishoni mwa wiki katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Pluijm ambaye ni kocha wa zamani wa Yanga SC, amedai kikosi chake kinahakikisha kinapata ushindi kila mechi hivyo anaumiza kichwa kwa Azam kwakuwa timu hiyo hadi sasa haijaruhusu hata bao lakini amewapa maelekezo ya kutosha wachezaji wake ili waweze kufunga watakapokutana.
Mpaka sasa Singida United inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi tisa lakini Azam FC wao wanakamata nafasi ya pili wakiwa na pointi kumi na hawajaruhusu nyavu zao kutikiswa lakini wamefunga magoli matatu tu.
Kocha wa Singida United anajivunia safu yake ya ushambuliaji kwani hadi sasa imeshafunga mabao matano ambayo yanawapa jeuri ya kushinda mbele ya Azam FC Jumamosi ijayo