YANGA YAPATA USHINDI MWEMBAMBA, NGOMA AUMIA TRNA

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Yanga SC leo imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC "Wanakuchele" katika mchezo mkali wa kusisimua uliopigwa jioni ya leo Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi nane ikiwa sawa na mahasimu wao Simba, goli pekee la ushindi la mabingwa hao watetezi lilifungwa na Ibrahim Ajibu akiunganisha krosi ya beki Kevin Yondan ambaye alitumia vema mpira wa kona alioanzishiwa na Juma Abdul, hata hivyo mshambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma aliumia na kutolewa nje ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Emmanuel Martin.
Ndanda leo wamecheza vizuri na kuipania Yanga ambapo kama si mabeki wa Yanga kuwa wajanja na kudhibiti mashambulizi ya Ndanda huenda mchezo huo ungeamuliwa na sare, Ndanda walikosa mabao ya wazi, kiungo wa Yanga, Mkongoman Papy Kabamba Tshishimbi alionyeshwa kadi ya njano ya tatu mfululizo na atakosekana katika mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Ibrahim Ajibu aliyefunga bao la ushindi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA