Kipa bora wa Airtel Rising Star apata shavu Qatar
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Kipa bora wa mashindano ya vijana ya Airtel Rising Star, Alfan Romanus amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Qatar ambapo tayari timu ya Spays Academy tayari inamuhitaji.
Akizungumza na Mambo Uwanjani, Romanus ambaye aliibuka kuwa kipa bora wa mashindano hayo, anatazamiwa kuondoka Oktoba 20 mwaka huu tayari kabisa kuanza majaribio yake.
Endapo Romanus atafuzu majaribio hayo atakuwa ameungana na Mbwana Samatta, Farid Mussa, Thomas Ulimwengu, Elius Maguli, Simon Msuva na Abdi Banda ambao wanacheza soka la kulipwa ughaibuni