LWANDAMINA ACHEKELEA KUREJEA KWA TAMBWE KIKOSINI

Na Saida Salum. Dar es Salaam
Kocha mkuu wa mabingwa wa soka nchini, Yanga SC, Mzambia George Lwandamina, amefurahia kurejea kwa straika Amissi Tambwe raia wa Burundi katika kikosi chake.
Tambwe alikosekana kwa muda mrefu baada ya kuumia mazoezini visiwani Pemba wakati Yanga ilipoenda kuweka kambi kujiandaa na mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao Simba.
Lwandamina amefurahia urejeo wa Tambwe kwakuwa ni mahiri kwa kufunga hivyo kikosi chake kitakuwa kikipata matokeo mazuri, Yanga imekuwa ikishinda ushindi mwembamba hivyo Tambwe anaweza kuwapa raha mashabiki wa Yanga.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Vital'0 ya Burundi na Simba ya Tanzania, amewahi kuwa mfungaji bora wa VPL mara mbili akiwa Simba alichukua ufungaji bora kwa kufunga magoli 19 na Yanga aliweza kufunga magoli 21, Tambwe ameanza mazoezi mepesi na huenda akawemo katika kikosi cha Yanga kitakachocheza na Mtibwa Sugar Jumamosi ijayo
Amissi Tambwe amerejea kikosini Yanga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA