Mji Njombe yafufuka Songea
Na Paskal Beatus. Songea
Baada ya kuondokewa na kocha wake mkuu Hassan Banyai, leo timu ya Njombe Mji FC ya mkoani Njombe imepata ushindi wake wa kwanza baada ya kuilaza Majimaji bao 1-0 katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Bao pekee la Njombe Mji limefungwa na Jimmr Shoji, matokeo mengine ya ligi hiyo ni kama ifuatavyo, Mwadui FC 1, Tanzania Prisons 3 (Mwadui Stadium, Yanga 1 Ndanda FC 0, kesho Jumapili ligi hiyo itaendelea tena kwa mechi nne kupigwa.
Azam FC wataialika Lipuli katika uwanja wao wa Azam Complex pale Chamazi, wakati Ruvu Shooting watawakaribisha Mtibwa Sugar, Stand United watawaalika Mbeya City pale Kambarage Syadium na Singida United watachuana na Kagera Sugar uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma