CAF YAIPOKA KENYA UENYEJI WA CHAN
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam
Shirikisho la kabumbu Barani Africa CAF limeinyang'anya uenyej wa Fainali za Mataifa barani Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) Kenya ambapo ilipangwa kufanyika nchini humo mwakani 2018.
CAF imeingiwa na hofu Kutokana Na Miundo Mbinu ya Nchi hiyo kutoridhisha na Pia Ukarabati wa Viwanja Haujakamilika hadi Sasa.
Hilo ni funzo kwa nchi zinazopewa nafasi ya kuandaa fainali za michuano mbalimbali ya CAF kuwa makini kukamilisha miundo mbinu yake ili yasije kutokea kama kwa Kenya ambao walipewa nafasi hiyo