ANCELOTTI AFURUSHWA BAYERN MUNICH

Kocha wa mabingwa watetezi wa Bundesliga Bayern Munich, Carlo Ancelotti ametimuliwa, ikiwa ni siku moja baada ya kufungwa mabao 3-0 na PSG kwenye ligi ya mabingwa Ulaya, “ Champions League”.

Ancelloti alijiunga na Bayern msimu uliopita na kuchukua ubingwa wa Bundesliga, lakini aliondolewa katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa ya 2016/17 na Real Madrid.

Inasemekana kutimuliwa kwake kumetokana na kuondoshwa huko katika michuano hiyo mikubwa Ulaya kwani kiu kubwa kwa mashabiki wa Bayern ilikuwa ubingwa wa Ulaya na matumaini ya timu hiyo yameyeyuka

Carlo Ancelotti amefutwa kazi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA