YANGA NA NDANDA NI KUFA NA KUPONA

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa mechi nne kupigwa katika miji tofauti, lakini mpambano unaovuta hisia za wengi ni kati ya mabingwa watetezi Yanga na Ndanda FC "Wanakuchele" wamakonde wa kutoka Mtwara.
Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jiji la Wazaramo kuanzia saa kumi jioni huku timu zote zikihaha kusaka ushindi, Yanga ambao ni mabingwa watetezi wanataka kushinda ili kuikamata Simba yenye pointi nane.
Yanga inataka kushinda mchezo huo ili kuwafurahisha mashabiki wake hasa baada ya kulazimishwa sare na Majimaji ya kufungana bao 1-1 katika uwanja wa Majimaji mjini Songea sare ambayo ilizua minong' ono ya hapa na pale
Yanga wanacheza na Ndanda jioni ya leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA