Ligi Kuu Bara kuendelea tena mwishoni mwa wiki
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Baada ya leo kuchezwa mchezo mmoja wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam na Mbao FC ya Mwanza uliopigwa katika uwanja wa CCM Kirumba na timu hizo kutoka sare ya kufungana mabao 2-2.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi na Jumapili kwa timu zote kukutana na kukamilisha mzunguko wa nne.
Jumamosi ni, Yanga Vs Ndanda FC, Uhuru Stadium, Singida Vs Kagera Sugar. Jamhuri mjini Dodoma, Mwadui FC Vs Prisons. Mwadui Shinyanga na Majimaji Vs Njombe Mji. Majimaji Songea.
Jumapili, Ruvu Shooting Vs Mtibwa Sugar, Mabatini, Mlandizi, Stand United Vs Mbeya City. Kambarage, Shinyanga na Azam Fc Vs Lipuli Fc. Azam Complex Dar es Salaam