TID kugombea Ubunge mwaka 2020
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Mwanamuziki maarufu wa Bongofleva, Khalid Mohamed "TID" amesema atawania ubunge ifikapo mwaka 2020 endapo atapata ridhaa kutoka kwa wazee.
TID ameyasema hayo asubuhi ya leo akihojiwa na Efm ambapo amedai atagombea nafasi hiyo endapo wazee watampa baraka zote, TID amedai atagombea ubunge katika jimbo la Kinondoni ambapo ndipo anapoishi.
Msanii huyo aliyepata kutamba na nyimbo mbalimbali ikiwemo "Zeze", "Siamini" na nyinginezo, amewahi kutuhumiwa madawa ya kulevya na alikamatwa katikati ya mwaka huu na kufunguliwa mashitaka na serikali kuhusu matumizi ya dawa hizo yeye na wasanii wenzake