MANJI AWAAHIDI NEEMA WACHEZAJI YANGA,ASEMA ANARUDI
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Aliyekuwa mwenyekiti wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC, Yusuf Mehbood Manji amewaahidi neema wachezaji wote wa Yanga na amedai haitachukua muda mrefu ataanza kuisaidia timu hiyo. Wachezaji wa Yanga na viongozi wao wote waliungana na Manji katika mahakama ya Kisutu juzi ambapo bosi huyo wa Quality Group alifikishwa hapo kujibu shitaka la kutumia dawa za kulevya, baada ya kuhairishwa kesi hiyo.
Manji aliketi na nahodha wa Yanga, Nadir Haroub "Cannavaro" ambapo kati ya maneno waliyozungumza yamenaswa kuwa ni kumtaka mwenyekiti huyo wa zamani arejee kuokoa jahazi kitu ambacho alikubali.
Manji alijiuzuru uenyekiti Yanga baada ya kuandamwa na matatizo na serikali kabla ya kufutiwa kesi yake ya kuhujumu uchumi hivyo sasa yuko huru na amewaambia wachezaji wa Yanga kwamba atarejea na raha zote zitarejea kama ilivypkuwa hapo nyuma.
Wachezaji wa Yanga jana waligomea mazoezi katika uwanja wa Uhuru na inasemekana wanaidai klabu hiyo mishahara ya miezi miwili, lakini Manji aliwapigia simu na kuwaomba warejee kazini atawapa noti