RATIBA YA LIGI KUU BARA MWISHONI MWA WIKI HII HAPA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea tena mwishoni mwa juma hili ambapo karibu timu zote zitashuka viwanjani kukamilisha mzunguko wa tano wa ligi hiyo inayoshika kasi.
Tayari timu tatu zinachuana juu kileleni huku kwa mara ya kwanza miamba Simba na Yanga zikiondoshwa katika kinyang' aanyiro hicho, mchuano huo unahusisha Mtibwa Sugar ambao ni vinara, Azam FC na Singida United
Ratiba hiyo inaonyesha Jumamosi kutachezwa mechi saba na Jumapili itachezwa mechi moja, ebu itazame ratiba kamili.
Jumamosi Septemba 30
Majimaji FC vs Kagera Sugar, (Majimaji Stadium, Songea)
Singida United vs Azam FC, (Jamhuri Stadium, Dodoma)
Ndanda FC vs Lipuli FC, (Nangwanda Stadium, Mtwara)
Yanga SC vs Mtibwa Sugar, (Uhuru Stadium, Dar es Salaam)
Mwadui FC vs Mbeya City, (Mwadui Complex, Shinyanga)
Mbao FC vs TZ Prisons, (CCM Kirumba, Mwanza)
Ruvu Shooting vs Njombe Mji FC, (Mabatini Stadium, Mlandizi)
Jumapili Oktoba 1
Stand United vs Simba SC, (CCM Kambarage Stadium, Shinyanga)