VICENT KIGOSI "RAY" AULA KAMATI YA MASOKO YANGA
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Kaimu mwenyekiti wa mabingwa wa soka nchini, Yanga SC, Clement Sanga ametangaza kuunda kamati saba zitakazoshughurika na masuala ya maendeleo katika klabu hiyo huku msanii maarufu wa filamu hapa nchini.
Vincent Kigosi maarufu Ray akitajwa kwenye kamati ya masoko kama mjumbe. Sanga ametangaza kuunda kamati saba jioni ya leo alipozungumza na waandishi wa habari huku majina ya wachezaji wa zamani wa klabu hiyo nao wakitajwa, pia mbali na msanii Ray kutajwa.
Msanii mwingine Haji Mboto naye ametajwa kwenye kamati hiyo, Ray na Mboto ni wakereketwa wakubwa wa Yanga hivyo kuwemo kwao kwenye kamati hiyo kutasaidia kukua kwa soko la Yanga katika masuala ya kuvutia wawekezaji.
Wachezaji wa zamani ambao wamejumuhishwa kwenye kamati zilizotajwa ambazo ni za kushughurika na masuala ya uwanja wa Kaunda, jengo la mtaa wa Mafia, masoko, Ufundi na nyinginezo ni Aoron Nyanda, Charles Boniface Mkwasa, Kenneth Mkapa, Mohamed Hussein "Mmachinga", Edibily Lunyamila, Abeid Mziba, Said Maulid "SMG" na wengineo