Mbeya City wapata kocha mpya

Na Exipeditor Mataruma. Mbeya
Wagonga nyundo wa Mbeya City wa jijini Mbeya hatimaye wamemtangaza kocha wao mpya baada ya kuachana na Mmalawi, Kinnah Phiri hivi karibuni.
Taarifa iliyotolewa jana usiku na uongozi wa timu hiyo umesema umemsainisha mkataba wa mwaka mmoja aliyewahi kuwa mshauri wa ufundi katika timu ya taifa ya Burundi Nsanzurwino Ramadhan kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Ramadhan amewahi pia kufundisha soka katika nchi za Rwanda, Kenya, Afrika Kusini na Burundi pia.
Mrundi huyo sasa anakuwa kocha wa tatu kuinoa timu hiyo baada ya Juma Mwambusi na Kinah Phiri, Mohamed Kijuso ambaye zamani amewahi kuichezea Simba SC ataendelea kuwa kocha msaidizi
Nsanzurwino Ramadhan, kocha mpya wa Mbeya City

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA