Mzee Akilimali asema, Clement Sanga anaihujumu Yanga
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Katibu wa Baraza la wazee la klabu ya Yanga, mzee Ibrahim Akilimali amesema kwamba, makamu kaimu mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga anaihujumu timu hiyo isifanye vizuri katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.
Akilimali ameyasema leo katika kipindi cha michezo cha Efm asubuhi, amedai Sanga amejiweka pembeni wakati timu ikiwa katika kipindi kigumu inachopitia.
Amedai kiongozi huyo anataka kuona Yanga inashuka daraja ili lawama zote abebeshwe mzee Akilimali ambaye alimkataa Manji na sera yake ya kuikodisha Yanga.