Mtibwa Sugar yashikwa na Ruvu Shooting lakini bado vinara Ligi Kuu Bara
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Licha ya Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli FC bao likifungwa na Mbaraka Yusuph usiku huu katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, lakini Mtibwa Sugar wameendelea kubaki kileleni ingawa jioni ya leo imebanwa na maafande wa Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani baada ya kufungana bao 1-1.
Mtibwa Sugar ililazimika kusawazisha baada ya Zubeir Dabi wa Ruvu kutangulia kufunga kabla ya Stamili Mbonde kukomboa. Mechi nyingine zilipigwa ambapo Stand United ilipata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Mbeya City 2-1 uwanja wa Kambarage wakati Singida United imeifunga Kagera Sugar 1-0.
Bao pekee la Singida United lilifungwa kwa mkwaju wa penalti na Mzimbabwe Tafadzwe Kutinyu na sasa Singida United chini ya Mholanzi Hans Van Pluijm sasa imefikisha pointi tisa ikiwa katika nafasi ya tatu nyuma ya vinara Mtibwa wenye pointi 10, Azam FC nafasi ya pili nao wana pointi 10 huku Prisons ikikamata nafasi ya nne na Simba na Yanga zinafuata