YANGA BILA TAMBWE TENA KUWAVAA NDANDA KESHO

Na Saida Salum. Dar es Salaam
Yanga SC itaendelea kumkosa mshambuliaji wake hatari Amissi Joselyin Tambwe raia wa Burundi katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhdi ya Ndanda FC Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Tambwe amekosa mechi tatu sasa na kesho pia ataendelea kukaa nje akiuguza majeraha ya goti na daktari wa Yanga, Edward Bavu anathibitisha kuwa Yanga ina majeruhi mmoja tu ambaye ni Tambwe, lakini Dissmas Ten ambaye ni msemaji wa klabu hiyo amedai ushindi ni lazima.
Yanga inahitaji ushindi ili kufikisha pointi nane na kuisogelea zaidi Simba ambayo jana ilishikwa shati na Mbao FC kwa kufungana mabao 2-2 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Ten amedai washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Thabani Kamusoko na Ibrahim Ajibu wana kila sababu ya kuhakikisha Yanga inapata matokeo mazuri na kujiimarisha katika msimamo wa ligi

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA