Mourinho kutoadhibiwa tena na FA
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho hatochukuliwa hatua zaidi baada ya kutimuliwa uwanjani na mwamuzi Claig Pawson Jumamosi wakati timu yake ilipocheza EPL.
Taarifa zaidi kutoka kwa Shirikisho la mpira wa miguu FA limesema adhabu ya kukosa mechi mbili kwa mkufunzi huyo inatosha na hawatamuadhibu tena.
Wengi walitegemea Mourinho angepata adhabu kubwa zaidi ya kufungiwa lakini FA imesema hatoadhibiwa tena kwani kifungo cha kukosa mechi mbili ni kikubwa kwake