ZFA YAISHIKA PABAYA TFF KUHUSU UTEUZI WA TIMU YA TAIFA

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) kimelishutumu Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania, (TFF) kwa kutoshirikisha wachezaji wa Zanzibar kwenye uteuzi wa timu ya taifa, Taifa Stars na kumshangaa kocha mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga akiita wachezaji 22 bila kuwemo wachezaji kutoka visiwani humo.
Zanzibar imeondolewa uanachama wake na Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, (CAF) kwa vile ni sehemu ya Tanzania hivyo haitaweza kushiriki michuano ya mataifa Afrika yanayoshirikisha timu za taifa.
Kwa maana hiyo wanatakiwa kuunda timu moja ya taifa kupitia jamhuri ya muungano, lakini Zanzibar wanatengwa na TFF na wameamua sasa kuishutumu hadharani TFF na wanataka kukutana na Rais wa Shirikisho hilo ili kuzungumzia kero hiyo.
Akizungumza leo, makamu wa Rais wa ZFA, Ally Mohamed amesema umefika wakati sasa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars atembelee visiwani na kuteua wachezaji kupitia ligi yao na si kukimbilia wavhezaji wanaocheza Simba,Yanga, Azam au Mtibwa wakati ligi ya Zanzibar ina wachezaji wazuri.
Hata hivyo Mohamed na ujumbe wake umepanga kuja Dar es Salaam kukutana na Rais wa TFF, Wallace Karia ili kuweka mambo sawa kwani Zanzibar inabaguliwa mno
ZFA wameishika pabaya TFF

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA