YANGA MGUU SAWA KUUA MTIBWA KESHO

Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga SC imewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani kesho watawapa furaha pale watakapoichakaza Mtibwa Sugar katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Habari na mawasiliano, Dissmas Ten amesema kikosi kipo tayari kuvaana na Mtibwa Sugar na amedai ushindi utapatikana kwani maandalizi yamekamilika.
Yanga ikiwategemea zaidi washambuliaji wake Donald Ngoma, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajibu, Emmanuel Martin na Thabani Kamusoko itataka kuwathibitishia mashabiki wake kuwa wataibuka na ushindi ili angalau kusogea mbele kwenye msimamo wa ligi.
Yanga itamkosa kiungo wake mkabaji, Mkongoman Papy Kabamba Tshishimbi ambaye ana kadi tatu za njano, Rekodi zinaonyesha Yanga imekuwa ikipata matokeo mazuri inapokutana na Mtibwa katika uwanja wa Taifa ama Uhuru jijini Dar es Salaam
Yanga SC wapo tayari kuilaza Mtibwa kesho

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA