Vita ya matajiri wawili VPL yamalizwa kwa sare
Na Mwandishi Wetu. Dodoma
Matajiri wawili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Singida United na Azam FC iliamuliwa kwa sare ya kufungana bao 1-1 jioni ya leo katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Singida United inayonolewa na Mholanzi Hans Van der Pluijm ilitangulia kupata goli la uongozi lililofungwa na Mrwanda, Danny Usengimana, lakini Azam wakakomboa kupitia Peter Paulo na kufanya timu hizo zigawane pointi moja moja.
Kwa matokeo hayo, Azam FC inaendelea kukamata nafasi ya pili ikifikisha pointi 11 ikishika dimbani mara tano, na kushinda mechi tatu, sare mbili, wakati Singida inakamata nafasi ya tatu na pointi zake 10 ikishinda mechi tatu, kufungwa moja na sare moja.
Matokeo mengine Ligi Kuu bara kama ifuatavyo. Mwadui FC 2 Mbeya City 2. Mwadui Complex. Shinyanga. Mbao FC 1 TZ Prisons 1, CCM Kirumba. Mwanza. Majimaji 0 Kagera Sugar 0. Majimaji Stadium. Songea. Ruvu Shooting 1 Njombe Mji 1. Mabatini Stadium. Mlandizi. Ndanda 2 Lipuli 1. Nangwanda Sijaona. Mtwara. Yanga 0 Mtibwa Sugar 0. Uhuru Stadium. Dar es salaam