Ajibu, Manyika warejeshwa tena Stars

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Salum Shaaban Mayanga amemresha tena mshambuliaji Ibrahin Ajibu wa Yanga na kipa Peter Manyika wa Singida United katika kikosi chake kitakachojiandaa na mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na FIFA, dhidi ya Malawi Oktoba 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Katika kikosi hicho, Mayanga ameita wachezaji watano wa kimataifa ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya Tanzania , kikosi cha Stars kinaundwa na makipa, Aishi Manula {Simba SC), Ramadhan Kabwili (Yanga SC) na Peter Manyika (Singida United).

Mabeki ni Gardiel Michael (Yanga SC), Boniphace Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kevin Yondan (Yanga SC), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC), Adeyun Ahmed (Kagera Sugar).

Viungo ni Himid Mao ambaye ni nahodha msaidizi, (Azam FC), Hamisi Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Muzamil Yassin (Simba SC), Raphael Daudi (Yanga SC), Simon Msuva (Difaa El Jadida/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya), Morel Famalicao, (Ureno).

Washambuliaji ni Mbwana Samatta ambaye ni nahodha, (KRC Genk/Ubelgiji), Ibrahim Ajibu (Yanga SC), Mbaraka Yusuph (Azam FC, kikosi hicho kinanolewa na Mayanga ambaye ni kocha mkuu akisaidiwa na Fulgence Novatus, Ame Ninja huku Patrick Mwangata akiwafunza makipa na Danny Msangi (Meneja)

Ibrahim Ajibu amerejeshwa Stars

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA