Kichuya naye arejea mdogo mdogo kikosini

Na Mwandishi Wetu

Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba SC, Shiza Ramadhan Kichuya leo ameungana na wenzake katika mazoezi ya timu hiyo inayojiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Kichuya ameanza mazoezi lakini akiwa chini ya daktari wa klabu hiyo, mchezaji huyo aliumia katika mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Simba ikilazimishwa sare ya mabao 2-2 huku Kichuya akiwa mfungaji wa goli la kwanza la Simba.

Mchezaji huyo alitolewa nje baada ya kuumizwa na wachezaji wa Mbao, huenda akawemo katika kikosi kitakachoanza dhidi ya Stand United utakaofanyika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, Simba ina pointi nane na inahitaji ushindi ili kusonga mbele kwenye ligi hiyo

Shiza Kichuya ameanza mazoezi leo baada ya kuumia

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA