Ndanda waapa kuizuia Yanga kesho
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Wachezaji wa timu ya soka ya Ndanda FC "Wanakuchele" ya mjini Mtwara wameapa kuisimamisha Yanga SC katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam kesho Jumamosi.
Ndanda imekuwa ikiizuia Yanga mara kwa mara zinapokutana hivyo watafanya kweli hiyo kesho, Yanga ilitoka kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Majimaji mchezo uliofanyika mjini Songea na kuwafanya wafikishe pointi 5.
Kikosi hicho cha Wanakuchele, wameiambia Mambo Uwanjani kuwa mchezo wa kesho wameuchukulia umuhimu wa hali ya juu wakiamini watapata ushindi ili kuwapa matumaini mashabiki wao