Mtibwa Sugar waanza kuchonga

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Mtibwa Sugar kupitia kwa msemaji wao Tobias Kifaru amesema kikosi chake kitaondoka na pointi tatu dhidi ya Yanga na kuendelea kuongoza ligi.

Kifaru amesema amekiona kikosi cha Yanga kinavyocheza anadhani timu yake itapata ushindi mkubwa kwani Yanga si lolote si chochote na kwa uchezaji wao sidhani kama watapata hata sare siku hiyo.

Hata hivyo rekodi inaibeba zaidi Yanga kwani timu hizo kila zinapokutana hasa katika Uwanja wa Taifa ama Uhuru jijini Dar es Salaam ni Yanga pekee imekuwa ikipata matokeo mazuri hivyo inaipa ugumu Mtibwa kuelekea katika mchezo huo

Mtibwa Sugar wameanza tambo dhidi ya Yanga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA