Samatta amshukuru Mwaisabula

Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji katika klabu ya KRG Genk, Mbwana Ally Samatta amesema hatomsahau kamwe kocha wake wa zamani Kenny Mwaisabula "Mzazi" kwani ndiye aliyemsaidia kumpa ujasili mpaka leo hii amefikia kuwa staa mkubwa wa kuaminiwa na klabu kubwa kama Genk.
Samatta aliandika maneno hayo kupitia ukurasa wake wa facebook ambapo amemmwagia sifa kemkem Mwaisabula ambaye pia amewahi kuzifundisha Bandari Mtwara, Cargo na Yanga SC.
"Kennedy mwaisabula "mzazi" heshima yako sana najua unajua kuwa nakuheshimu ila inawezekana ujui ni kwa kiasi gani,umenijengea moyo mgumu na wenye kutokukata tamaa kila siku ktk soka kwa lile ulilolifanya wakati ule nikiwa bado mdogo kbsa.
"Siku ambayo sikulala usingizi nikihofia mechi baada ya "mzazi" kuniambia kuwa mechi ya kesho utaanza. Nadhan unaikumbuka taifa cup basi siku iyo ilikuwa "temeke na mbeya" wkt bado nipo mbagala market ata "harufu ya maziwa ya mama aijaniisha vyema" japo nilichemka kwny Ile mechi ila matunda yake yamekuja baadae asante Kennedy Mwaisabula nakushukuru kwa kuniamini kabla ata sikujiamini, asante sana "mzazi"
Kenny Mwaisabula "Mzazi", amekumbukwa na Mbwana Samatta
Mbwana Samatta amtaja Mwaisabula katika mafanikio yake

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA