Wachezaji Yanga warejea mazoezini
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Wachezaji wa mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC wamerejea mazoezini leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza mgomo wao baridi uliochukua siku moja.
Taarifa kutoka Jangwani zinasema wachezaji wamekubali kurudi mazoezini na uongozi unashughurikia malalamiko yao. Inasemekana wachezaji hao wanadai mishahara yao ya miezi miwili na ndio iliyopelekea mgomo huo.
Yanga Jumamosi ijayo itachuana na Ndanda FC katika muendelezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara katika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam