OKWI ALAMBA MILIONI MOJA YA UCHEZAJI BORA
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Mshambuliaji wa Simba SC, Emmanuel Okwi raia wa Uganda, amelamba kitita chake cha shilingi Milioni moja baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mshambuliaji huyo alishinda tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu yake kushinda mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting huku yeye akifunga mabao manne na kuseti moja.
Okwi aliwabwaga nyota wenzake wawili, Mohamed Issa wa Mtibwa Sugar na Boniface Maganga wa Mbao FC.