SIMBA WAAPA KUIMALIZA STAND UNITED KWAO
Na Paskal Beatus. Mwanza
Mabingwa wa Ngao ya Jamii, Simba SC wamesema safari hii hawatafanya makosa katika mchezo wao wa ligi dhidi ya Stand United utakaopigwa katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
Simba wanajifua jijini Mwanza ambapo wameweka kambi yao kwa ajili ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wake, Simba ilitoka kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Mbao FC mchezo uliofanyika uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Pia Simba ikaenda Tabora kucheza mechi ya kirafiki na Milambo na kulazimishwa sare ya 0-0, na mashabiki wa Simba wakaanza kumshutumu kocha Mcameroon, Joseph Omog ambapo wamekuwa wakitaka aondolewe, lakini uongozi wa Simba unamkingia kifua na mara kwa mara msemaji wa timu hiyo Haji Manara amekuwa akisema kocha huyo aondoki.
Kuelekea mchezo huo dhidi ya Stand United Jumamosi ijayo, msemaji wa timu hiyo Haji Manara amesema Stand United lazima ife nyumbani kwao kwakuwa wamejipanga kushinda mchezo huo na hakuna kitakachowafanya wasipate ushindi