MANJI AFUNGUKA MAZITO MAHAKAMANI, AKIRI KUTUMIA MADAWA
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Mehbood Manji amefunguka mambo makubwa mahakamani wakati wa kusikilizwa kwa shauri lake la kutumia madawa ya kulevya.
Manji ambaye alikamatwa na jeshi la polisi na kushikiliwa kwa muda amekiri ni kweli anatumia madawa ya aina ya Morphiem na Benzodiazepines ambazo zinamsaidia kwa matatizo ya moyo.
Manji amefunguka hayo katika mahakama ya Kisutu leo kuwa amekuwa akitumia dawa hizo kwa muda mrefu na zimekuwa zikimtibu maradhi ya moyo ambayo yamekuwa yakiitesa familia yao kwa miaka mingi na yeye aligundulika kuwa na ugonjwa huo tangu akiwa na miaka 26.
Aidha mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga amelilalamikia jeshi la polisi kwa kitendo chake cha kwenda kukagua nyumbani kwake na kuchukua kompyuta yake iliyokuwa na nyaraka za bisshara xake, Manji pia amesema mbali na kuchukuliwa kompyuta yake pia simu na vitu vyake vingine navyo vilibebwa na polisi hao na hadi sasa bado hajarudishiwa