Wachezaji Yanga wagomea mazoezi kisa hawajalipwa chao

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Hali si shwari katika klabu ya Yanga baada ya wachezaji wake kugomea kufanya mazoezi leo ya asubuhi mpaka jioni yaliyokuwa yafanyike Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam na kujikuta wakielekea makao makuu mtaa wa Twiga na Jangwani.

Yanga ilikuwa ifanye mazoezi yake leo ikiwa katika maandalizi yake ya Ligi Kuu Bara, inasemekana wachezaji wa Yanga walikataa kutelemka kwenye gari na kulazimika kufanya kikao na viongozi.

Hata hivyo inasemekana wachezaji hao wameamua kugomea mazoezi kisa wanadai mishahara yao isiyopungua ya miezi miwili, uongozi wa Yanga haukuwa tayari kuzungumzia hilo ambapo kila mmoja alikuwa akimtupia mzigo mwenzake

Wachezaji wa Yanga wamegoma kufanya mazoezi leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA