OKWI AKAMATIKI AISEE, AWAUA MWADUI YEYE NA BOCCO
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Simba SC imezidi kutoa vipigo vitakatifu baada ya jioni ya leo kuifanyia kitu mbaya Mwadui FC ya Shinyanga kwa kuichabanga bila huruma mabao 3-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Emmanuel Okwi "Muhenga" kama baadhi ya mashabiki wa mahasimu wao wanavyomuita, aliwainua vitini wapenzi na mashabiki wa Simba kwa kufunga mabao yake mawili safi huku nahodha, John Bocco "Adebayor" akitumbukiza moja na kuifanya Simba iibuke na ushindi huo mnono ikifikisha pointi saba na sasa inakamata nafasi ya pili.
Katika mchezo huo wa leo vijana wa Simba wamecheza soka zuri na kufurahisha mashabiki wake ambapo Mwinyi Kazimoto na Jonas Mkude wakicheza kwa mara ya kwanza