Uongozi Simba wamkingia kifua Omog
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Uongozi wa klabu ya Simba umesema kocha wake mkuu,Mcameroon,Joseph Marius Omog ataendelea kukinoa kikosi hicho.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari Haji Sunday Manara ambapo amedai kocha huyo ataendelea na kazi yake na si kama wanavyotaka baadhi ya mashabiki wa timu hiyo ambao hawana uvumilivu.
Manara amedai wapo baadhi ya mashabiki wanadhani kubadili makocha kila msimu ndio huleta mafanikio hilo si kweli na Omog atabaki kuwa kocha wa Wekundu hao ambao kwa sasa wanakamata nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba inajiandaa na mchezo wake ujao dhidi ya Mbao FC utakaofanyika jijini Mwanza kisha itaifuata Stand United mjini Shinyanga, awali mashabiki wa Simba walikuwa wakishinikiza kocha wao Joseph Omog aondolewe kwa sababu timu yao ilitoka suluhu na Azam FC