ALIYETAKA KUMTOA ROHO EMMANUEL MARTIN WA YANGA ASIMAMISHWA LIGI KUU
Na Shafih Matuwa. Dar es Salaam
Kamati ya masaa 72 ya Bodi ya uendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, leo imetoa hukumu mbalimbali na kufikia maamuzi ambapo imemsimamisha mchezaji wa Majimaji ya Songea, Juma Salamba kwa kitendo chake cha kumpiga kiwiko kiungo mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Martin katika mchezo wa ligi uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Martin ambaye aliingia kuchukua nafasi, alijikuta akipigwa kiwiko na kusababisha apoteze ufahamu wake wa akili (Kuzirai) ambapo alikimbizwa hospitali, Martin alikuwa msaada kwa Yanga katika mchezo huo ambapo kuingia kwake kulipelekea Yanga kusawazisha goli.
Salamba amesimamishwa na kamati hiyo huku kesi yake ikisikilizwa, Hata hivyo Martin amerejea tena uwanjani na anaendelea kuichezea timu yake, wakati Salamba akisimamishwa, mwamuzi wa mchezo huo naye amepewa adhabu kwa sababu alishindwa kumuonya mchezaji aliyemdhuru mwenzake uwanjani