Serikali yafuta Miss Tanzania na tuzo za Kill
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Serikali imefuta rasmi mashindano ya Miss Tanzania na yale ya kuwania tuzo za muziki za Kilimanjaro Music Award kwa madai zimekuwa zikiendeshwa kwa ubabaishaji mkubwa huku wanaoshinda inadaiwa wamekuwa wakipendelewa.
Hivyo sasa imeamua kuingilia kati na kusitisha mashindano yake na itapanga utaratibu mpya kabla hayajaanza upya, hayo yameamuliwa na wizara ya Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa kupitia kwa waziri wake Dk Harrison Mwakyembe.
Serikali imefikia maamuzi hayo baada ya kusikiliza malalamiko ya wadau juu ya uendeshaji wa mashindano hayo pamoja na kugubikwa na ubabaishaji katika utoaji wa zawadi kwa washindi, serikali imewataka waandaaji kuwasilisha zawadi kwao mapema kabla mashindano hayajaanza