Straika wa Stand United aula Zimbabwe
Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam. Mshambuliaji wa kimataifa wa Stand United, raia wa Nigeria, Chidiabere Abaslim hatimaye amefuzu vipimo vya afya na kusajiliwa na mabingwa wa soka nchini Zimbabwe, Caps United kwa kandarasi ya miaka miwili. Chidiabere aliyewahi pia kuichezea Coastal Union ya Tanga ambayo akashuka nayo daraja kabla ya kurejea Stand United timu ambayo ilimuibua kisoka tangu alipojiunga nayo mwaka 2014. Mshambulizi huyo alikuwa na mwanzo mzuri msimu wake wa kwanza akiwa Stand United ambapo aliweza kuchuana na vinara wa magoli Ligi Kuu Bara, Coastal Union waliamua kumchukua ili awasaidie lakini kwa bahati mbaya Chidiabere aliumia na akashindwa kuisaidia timu hiyo isishuke daraja. Kwa maana hiyo Chidiabere atakuwepo kwenye kikosi cha mabingwa hao watakaposhiriki michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani kwani timu hiyo ndio mabingwa wa Zimbabwe