OKWI ASAINI SIMBA MIAKA MIWILI

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Kiungo mshambuliaji Emmanuel Okwi raia wa Uganda amesaini kandarasi ya miaka miwili kujiunga na Simba SC msimu ujao huku akifunguka mengi na kudai atauwasha moto kwenye ligi kuu.

Okwi anajiunga na Simba kwa mara ya tatu baada ya kufanya hivyo akitokea SC Villa ya kwao Uganda aliyojiunga nayo akitokea Denmark katika klabu ya Sonderjyske inayoshiriki Ligi Kuu.

Mshambuliaji huyo alivunja mkataba na timu hiyo baada ya kudaiwa kushuka kwa kiwango chake lakini Okwi amesema wasibiri ligi ianze auwashe moto, Naye mfadhili wa Simba, Mohamed Dewji "Mo" amesema yeye ndiye aliyefanikisha usajili huo na amedai ni zawadi kwa mashabiki wa Simba.

Okwi amesaini mkataba huo mbele ya makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange "Kaburu", Okwi alitua nchini jana usiku akitokea kwao Uganda

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA