Stars kupaa bondeni usiku

Na Salum Fikiri Jr

Timu ya taifa, Taifa Stars, inaondoka leo usiku wa saa moja na nusu kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo itashiriki michuano ya kombe la Cosafa ikiwa kama mwalika.

Alfred Lucas Afisa Habari wa Shirikisho la soka nchini (TFF) amesema kikosi cha timu ya taifa kinaondoka usiku wa saa moja na nusu hii leo kuelekea Afrika Kusini ambapo itashiriki michuano ya Cosafa.

Lucas amedai kikosi kikitoka Afrika Kusini kitarejea nchini kisha kitaanza maandalizi dhidi ya Rwanda kusaka tiketi ya kufuzu fainali za kombe la CHAN, hata hivyo Lucas amedai kikosi cha Stars kinachonolewa na Salum Mayanga kitafanya vizuri katika mashindano hayo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA