Mshahara wamwondoa Singano, Azam FC

Na Prince Hoza. Dar es Salaam

Dau nono litalotolewa na klabu ya Difaa El Jajida ya Morocco inadaiwa kumwondoa kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Ramadhan Singano "Messi" aliyekataa kuongeza mkataba mwingine.

Messi kama anavyofahamika na wengi, amekataa kusaini mkataba mpya na Azam ambayo imempunguzia dau na kuamua kugeukia dili ya Morocco ambapo ametamgaziwa mshahara mnono wa Dola 2000 kwa mwezi sawa na shilingi Milioni 4.4.

Uzushi unaoenea mitaani kuwa winga huyo wa zamani wa Simba na Taifa Stars kuhusishwa na mpango wa kurejea Simba si kweli, Messi hana mpango wa kurejea Simba isipokuwa amegomea mkataba mpya wa Azam na anataka kupaa zake majuu

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI