Musa Kisocky akalia kuti kavu Sputanza, mbinu chafu kumuondoa zasukwa
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Imefahamika kuwa mwenyekiti wa chama cha wanasoka, (SPUTANZA) Musa Kisocky yuko hatihati kung: olewa katika nafasi hasa baada ya katiba ya chama hicho kuwekewa mkazo kuwa mwenyekiti lazima awe amecheza soka tena Ligi Kuu.
Marekebisho ya katiba huenda yakafanywa hivi karibuni na inadaiwa ina njama za kumtoa mwenyekiti huyo aliyekaa madarakani kwa kipindi kirefu sasa.
Baadhi ya wanachama wa Sputanza wanasema Kisocky anakiongoza chama hicho lakini hana sifa kwakuwa hakucheza Ligi Kuu ingawa yeye mwenyewe amekuja juu.
Kisocky slipoulizwa alikiri ni kweli yeye hakucheza Ligi Kuu lakini amewahi kucheza ligi ambayo kwa miaka hiyo ilikuwa kuu, "Nimecheza mpira zamani kwenye timu ya Asante Tololi ya Dar es Salaam, zamani kulikuwa na ligi iliyojulikana kama klabu bingwa", alisema Kisocky ambapo aliwashangaa wanaompinga ambapo amedai kucheza Simba au Yanga ndiyo kunakowaaminisha watu