Sarah avunja rekodi ya usajili Liverpool
Timu ya Liverpool ya Uingereza imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji wa AC Roma ya Italia, Mohamed Salah kwa kumpa kandarasi ya miaka mitano kwa kuvunja rekodi ya mauzo Paundi Milioni 39.
Rekodi ya mauzo ya usajili iliwekwa na Andre Carol ya Paundi Milioni 35, kwa maana hiyo Sarah, raia wa Misri anakuwa mchezaji ghali kwenye kikosi hicho kitakachoshiriki Ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Hata hivyo Sarah amefurahia usajili wake wa kutua Anfield aliamini ataipa mafanikio timu hiyo iliyotwaa taji la ligi ya premia mara 18. "Nimefurahia kujiunga Liverpool, nitaitumikia kwa moja mmoja, naamini tutatwaa mataji", alisema Sarah alipotambulishwa rasmi