TANZANIA YATINGA ROBO FAINALI COSAFA CUP
Na Exipedito Mataruma. Rustenburg.
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya Mataifa ya ukanda wa kusini mwa Afrika, Cosafa Castle Cup baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Mauritius.
Mchezo huo uliokuwa mkali na wa kuvutia, Stars ilisawazisha bao kupitia kwa winga wake Simon Msuva aliyeingia kipindi cha pili.
Kwa matokeo hayo Tanzania inaungana na Botswana, Zambia, Namibia, Lesotho, Swaziland na Afrika Kusini kucheza robo fainali huku zikisubiria timu nyingine moja kutoka kundi B.
Katika mchezo mwingine wa kundi A, Angola ililazimishwa suluhu 0-0 na Malawi na kuifanya Tanzania isonge hatua nyingine kirahisi, Stars itakutana na mwenyeji Afrika Kusini, Bafana Bafana