Kimeeleweka, Ngoma asaini miwili Jangwani
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Baada ya kuzuka kwa taarifa kwamba mshambuliaji wa kimataifa raia wa Zimbabwe, Donald Ndombo Ngoma amesaini mkataba wa miaka mitatu katika timu ya Polokwane City ya Afrika Kusini, hatimaye amemaliza ubishi baada ya mchana wa leo kusaini mkataba wa miaka miwili na timu yake ya Yanga SC.
Ngoma pia alikuwa akihitajika na mahasimu Simba, lakini ameamua kumalizana na timu yake aliyoitumikia misimu miwili kwa mafanikio makubwa akiipa ubingwa wa bara mara mbili, kombe la FA, Ngao ya Hisani pamoja na kuiwezesha kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.
Ngoma alisajiliwa na Yanga akitokea FC Platinum ya kwao Zimbabwe amekuwa mmoja kati ya washambuliajj nyota ambao waliweza kutolewa udenda na vilabu mbalimbali barani Afrika