Kichuya aibeba Stars, Cosafa
Na Exipeditor Mataruma. Afrika Kusini.
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jioni ya leo imefanikiwa kuanza vema michuano ya Cosafa baada ya kuilaza timu ya taifa ya Malawi kwa mabao 2-0 mchezo wa kwanza kundi A.
Stars ilijipatia mabao yote mawili katika kipindi cha kwanza yote yakifungwa na Shiza Ramadhan Kichuya kipindi cha kwanza mabao ambayo yaliipa ushindi Stars na kuanza vema michuano hiyo tofauti na mwaka jana ilipoondolewa mapema.
Mchana kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga alisema lazima kikosi chake kitachomoza na ushindi kwakuwa Malawi anawafahamu vizuri, Stars itashuka tena dimbani Jumanne kukwaruzana na Angola ambao leo wanachuana na Mauritius